Connect with us

Subscribe

Subscribe

Music

Abigail Chams Awakutanisha Marioo, Rayvanny, Whozu Na Chino Kid Kwenye Muziki Mpya ‘5’

Mwanafamilia wa Sony Music East Africa, Abigail Chams, Ijumaa (Septemba 29) ameiachia EP yake ‘5’ yenye nyimbo sita ikiwa na kolabo kutoka kwa Marioo, Rayvanny, Whozu na Chino Kid. Nyimbo za kwenye ‘5’ zimetengenezwa na S2Kizzy, Sound Boy na Abbah.

5 inaweka rekodi ya kuwa EP ya kwanza kwenye historia ya muziki wa Abigail Chams ambaye ni miongoni mwa wasichana wadogo wanaofanya maajabu kwenye Bongo Fleva. Abby amewekeza uwezo mwingi kwenye kuhakikisha anafanya kile ambacho mashabiki wa Bongo Fleva wamekuwa wakitamani kusikia kutoka kwa muimbaji wa kike.

 Abby ameiambia SnS kuwa, namba 5 ndiyo namba yake pendwa, inamuhusu kwenye mambo yake mengi ikiwemo kuanza kujifunza vyombo vya muziki akiwa mtoto wa miaka mitano na sababu nyingine nyingi  zilizomfanya kuiita EP yake ya kwanza 5.

Wimbo namba moja kwenye 5 ni ‘Falling In Love’. Wimbo huu wenye urefu wa dakika 3:32, umebeba hadithi ya mapenzi inayomuhusu msichana anaefikri kama anaanza kuzama kwenye mapenzi. Msichana huyo anaikumbuka siku ambayo hawezi kuisahau baada ya kukutana na mvulana aliyeanza kuuteka moyo wake. “Ilikuwa tarehe 17, mwezi wa julai mwaka jana, tarehe tuliyokutana, tarehe siwezi kuisahau.” Abby anaimba kuanzia sekunde ya 45 ya wimbo huu. Kwenye wimbo huu, Abby anasimulia jinsi ambavyo anaogopa kufanya maamuzi hata baada ya marafiki kumshauri. Ni wazi kuwa wimbo huu utakuwa wimbo pendwa kwa wasichana sana na utatumika kwenye kuchochea ushawishi kwa wale wanaofikiria kuanzisha ‘penzi jipya’.

March 17 mwaka huu, Abby aliiachia kolabo yake na Marioo, ‘Nani’ kama wimbo wa kwanza kusikika kutoka kwenye 5. Nani umeacha rekodi kadhaa za Marioo na Abigail Chams ikiwemo rekodi ya wimbo wao unaopendwa na mashabiki wa Bongo Fleva.  Siku chache baada ya Nani kuachiwa, Abigail Chams na Marioo walipata mwaliko kuhudhuria The Dotty Show inayorushwa na Apple Music. Video ya wimbu huu inashikira rekodi nyingine ya kuwa video ya kwanza na pekee kutoka kwa Abigail iliyofikisha zaidi ya watazamaji milioni moja YouTube.

Kolabo hii ya kwanza kati ya Abby na Marioo, imepewa namba mbili kwenye EP hii yenye jumla ya nyimbo sita.

Wimbo namba tatu kwenye 5 ni Milele ambao uliachiwa baada ya miezi sita ya mafanikio ya Nani. Kwa mujibu wa Abby, wimbo huu uliandikwa maalum kwa ajili ya wazazi wake ambao wamedumu kwenye ndoa kwa miaka 25. Wimbo huu unaturudisha kwenye ‘Falling In Love’, baada ya kuzama kwenye mapenzi, hakuna kitu mtu anaweza kusubiri badala ya kuliombea penzi kuwa la milele. Abby ameitumia sauti yake kuongea kwa niaba ya wapenzi ambao walihisi labda hawana maneno ya kuambia wapenzi wao. Milele ni wimbo bora wa mapenzi ambao utadumu, maudhui ya wimbo huu yanalenga zaidi kwenye kuutunza upendo. Matamshi ya Abby kwenye wimbo huu ni maneno ya watu wanaojua maana halisi ya upendo.

Akiongea na SnS, Abby amesema kuwa ameandika maneno ya wimbo huu kwa asilimia 70 huku Abbah akihusika kwenye uandishi wa wimbo huu kwa asilimia 30. Abigail amemtaja Abbah kama producer wa Tanzania mwenye ufahamu mkubwa na muziki na amekuwa akifurahia kufanya nae kazi.

Wimbo uliopewa namba nne kwenye 5 EP, ni Corazon akiwa ameshirikishwa Rayvanny. Kwa mujibu wa Abigail, wimbo huu ulirekodiwa siku nyingi wawili hao walipovutiwa na mdundo wa Sound Boy.

Abigail alimuambia Sky wa SnS kuwa, Rayvanny amekuwa sehemu ya watu wanaomuongoza vizuri kwenye kiwanda cha muziki tangu akliwa anaanza.

Corazon unaweka hesabu ya kuwa kolabo yao ya pili baada ya Stay wa Rayvanny uliotoka 2021.

Tano bora ya 5 EP inafungwa na Bata, kwenye wimbo huu Abby amekuja na wimbo wa kuchangamsha watu linapokuja suala la kufurahi. Kama ambavyo wimbo wenyewe unaitwa ‘Bata’, Abby anasimulia mambo mengi ya kutufanya tufurahie maisha haya ambayo tunayaishi mara moja.

Bata ni stori inayokukumbusha kuwa, unaweza kujiachia unavyotaka lakini usiache kumuogopa Mungu.

Pombe nakunywa, bata nakula, kote navuma na ninamuogopa Mungu.
Nimeshajipata niacheni nijidai
. Inasikika sauti ya Abby akiimba mahali fulani kwenye wimbo huu. Sauti nyingi zinazosikika kwenye wimbo huu ni sauti za Abby Chams, Gabrielle Chams ambaye ni meneja wake, Abbah pamoja na Jaivah.

Baada ya kuzisikiliza tano zote, sasa ni wakati wa kufunga kurasa ya EP hii na moja ya mwisho. Wimbo namba sita ‘Chapati’, ambayo ni kolabo ya kwanza ya Abigail inayowakutanisha Whozu na Chino Kid. Chapati ni wimbo unaowakutanisha mtu na Ex wake wakitambiana kuhusu wapenzi wao wapya. Whozu amefanya kazi kubwa kwenye korasi ya wimbo huu. ‘Umempata mpenzi lakini hawezi kunifika’, Ukiisikia hii inapigwa uwanja wa Bata, itakunyanyua ujiachie na kuonyesha mbwembwe zako hata kama hakuna Ex wa kumtambia.

Newsletter Signup

Written By

Enky Frank is An Entertainment Commentator & Writer, Writing More About The People Who Shape The Music Industry. With Ten years Of Experience, Enky's Articles Have Been Published In SnS, Global Publishers, Gazeti La Makorokocho, lilOmmy.com, Diva255.co & Elsewhere.

1 Comment

1 Comment

  1. Pingback: ‘5 EP’ Ya Abigail Chams, Siku Tatu Za Kwanza Zinatafsriwa Vipi? - Simulizi na Sauti

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Entertainment

Jinsi dawa za kulevya zinavyoharibu maisha ya Britney Spears, muziki wake na ‘boyfriend’ atajwa kuwa tatizo: wasanii wetu wa kike kuna cha kujifunza?

Lifestyle

Shirika la Bima China laweka nia ya Kugharamia Reli ya Kisasa

Finance

From FaceBook to Meta:12 Years Of Transformation

International

Left to Right: Company Secretary, Mr. Bili Odum; Executive Director,/GCOO, Mr. Alex Alozie; Group Head, Marketing and Corporate Communication, Ms Alero Ladipo; Group Managing Director/CEO; Mr. Oliver Alawuba; Group Deputy Managing Director, Mr. Muyiwa Akinyemi; and Executive Director, Mr. Ugo Nwaghodoh, at the Global Press Conference to herald the year-long celebration of UBA at 75, in Lagos on Monday Left to Right: Company Secretary, Mr. Bili Odum; Executive Director,/GCOO, Mr. Alex Alozie; Group Head, Marketing and Corporate Communication, Ms Alero Ladipo; Group Managing Director/CEO; Mr. Oliver Alawuba; Group Deputy Managing Director, Mr. Muyiwa Akinyemi; and Executive Director, Mr. Ugo Nwaghodoh, at the Global Press Conference to herald the year-long celebration of UBA at 75, in Lagos on Monday

UBA Celebrates 75 Years Of Banking Excellence, Marks 15 Years In Tanzania

Finance

Kuboresha Malipo ya Ada za Shule: Benki ya Exim Yazindua huduma ya ‘Exim Smart Shule’

Tech

President Samia Suluhu Hassan Extends Heartfelt Condolences to Iran Following President Raisi’s Tragic Death

International

Advertisement
Newsletter Signup

Copyright © 2024 Simulizi na Sauti. Sparkling Conversation.

Connect
Newsletter Signup

Subscribe for notification